Idadi ya visa vya maambukizi yakifika milioni 1.5 duniani
Imechapishwa:
Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona duniani imeongezeka na kufikia zaida ya Milioni 1.4, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani.
Pamoja na takwimu hizo, chuo hicho kinasema watu wengine 90,000 wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo.
Wakati huo huo, idadi ya watu waliofariki dunia nchini Uhispania imeongezeka na kufikia 15,200, licha ya ripoti kuwa kasi ya maambukizi sasa inapungua.
Katika kipindi cha saa 24 Jumatano hadi Alhamisi wiki hii; watu 5,756 waliambukizwa kutoka 6,180 siku ya Jumatano.
Bunge nchini humo linajadili uwezekano wa kuondoa marufuku ya kutotembea nje kutokana na maambukizi haya.
Wakati huu Shirika la afya duniani, WHO, likitoa wito wa serikali mbalimbali kuhakikisha kuwa watu wanapimwa, nchini Ufaransa serikali imeamua njia ya teknolojia kuwatafuta watu ambao huenda waliambukizwa.
Nalo, shirika la kimataifa linalotoa misaada ya linasema janga hili huenda litasababisha watu zaidi ya Milioni 500 kuwa maskini duniani.
Wakati huo huo Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva, ameonya kuwa ukuaji wa uchumi duniani utaanguka kabisa katika mwaka huu wa 2020, huku 170 kati ya nchi wanachama 180 wa IMF zikishuhudia kupungua kiwango cha mapato ya wastani.
Hata hivyo amezitaka serikali kuchukua hatua zaidi za kusaidia makampuni ya kibiashara ili kuepusha athari kwa uchumi na kufanya iwe vigumu kuufufua baada ya janga hili kumalizika.