AFRIKA MASHARIKI-FAO-KILIMO-UCHUMI

FAO: Afrika ya Mashariki hatarini kuvamiwa na nzige wa jangwani

Wakaazi wa Samburu wanajaribu kufukuzana na kundi la nzige katika kijiji cha Lemasulani, Kaunti ya Samburu, Kenya, Januari 17, 2020.
Wakaazi wa Samburu wanajaribu kufukuzana na kundi la nzige katika kijiji cha Lemasulani, Kaunti ya Samburu, Kenya, Januari 17, 2020. REUTERS/Njeri Mwangi

Tangu waonekane kwa mara ya kwanza nchini Somalia mwishoni mwa mwezi Desemba 2019, nzige wa jangwani wamevamia nchi kadhaa katika ukanda huo na kusababisha uharibifu mkubwa katika mashamba.

Matangazo ya kibiashara

Hali inaweza kuwa mbaya zaidi katika wiki zijazo ambapo kundi la nzige wa jangwani linatarajia kuvamia maeneo ya Kenya, Sudani Kusini na Uganda.

Kizazi kipya kinachodhuru zaidi

Mvua kubwa zilizonyesha mwezi Machi zinaweza kusababisha nzige wa jangwani kuongezeka Afrika Mashariki, kulingana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Hali ya hewa inaweza kusababisha wadudu wanakuwa wengi katika ukanda huo. Nzige wa jangwani wanaishi kwa miezi mitatu tu, lakini huzaana haraka. Nzige wa jangwani ambao waliwasili katika maeneo ya Afrika Mashariki mwishoni mwa mwaka wa 2019, walipata muda wa kutaga mayai mengi, na kizazi kipya kinaweza kuwa kikubwa na hatari zaidi kuliko kile cha awali.

Uharibifu Ethiopia

Wimbi la kwanza la nzige wa jangwani tayari wamesababisha uharibifu mkubwa katika nchi kadhaa zilizoathiriwa na uvamizi wa mabilioni ya wadudu hawa wanaotisha.

Nchini Ethiopia, hekta 200,000 za ardhi ya kilimo zimeharibiwa, na watu milioni moja sasa wanahitaji msaada wa chakula cha dharura, kwa mujibu wa FAO.