Pata taarifa kuu
WHO-DUNIA-CORONA-AFYA

WHO:Dunia ingelisikia na kufanyia kazi ushauri wetu kuhusu Covid-19, lakini walipuuzia

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kama Shirika hawana uwezo wa kuzilazimisha nchi kufuata ushauri wao.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kama Shirika hawana uwezo wa kuzilazimisha nchi kufuata ushauri wao. REUTERS/Denis Balibouse

Shirika la Afya Duniani WHO linasema kuwa lilitoa tahadhari ya mapema kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona lakini baadhi ya mataifa duniani, yalipuuza.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kama Shirika hawana uwezo wa kuzilazimisha nchi kufuata ushauri wao.

WHO inasema maambukizi ya Corona yatamalizika hivi karibuni, wakati huu dunia ikiwa na maambukizi zaidi ya Milioni 3 na watu zaidi ya 200,000 kupoteza maisha.

Hata hivyo hivi karibuni rais Marekani Donald Trump alililaumu shirika la Afya Duniani kwa kuegemea zaidi upande wa China.

Rais huyo wa Marekani alidai kwamba shirika hilo la kimataifa lilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Rais Trump alisema shirika hilo liliisifu China ingawa pana sababu ya kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi  iliyotolewa na serikali ya China juu ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya Corona.

Shirika hilo la kimataifa lililitangaza mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona kuwa hatari kwa afya ya binadamu wote, tarehe 30 mwezi Januari, takriban mwezi  mmoja kabla ya rais wa Marekani kusema kwenye "twitter” kwamba maambukizi ya virusi vya corona yalikuwa yamedhibitiwa nchini Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.