DUNIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yafikia 250,000 duniani

Ugonjwa wa Covid umesababisha vifo vya watu wengi dunia.
Ugonjwa wa Covid umesababisha vifo vya watu wengi dunia. REUTERS/Vasily Fedosenko

Idadi ya vifo vinavyohusiana na janga la Covid-19 imepindukia 250,000 duniani, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha nchini Marekani, huku kikiongeza kuwa maambukizi ya virusi vya Corona yamefikia zaidi ya milioni 3.5.

Matangazo ya kibiashara

Marekani ndio nchi inayoongoza kwa maambukizi na vifo, ambapo watu milioni 1.2 wamekwishaambukizwa nchini humo, huku wapatao 69,000 wakiwa wamekufa kwa ugonjwa huo.

Chuo hicho pia kimearifu kuwa takriban watu milioni 3.6 wamepata maambukizi ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya corona.

Hayo yanajiri wakati viongozi wa nchi za Ulaya wameahidi kuchangisha Euro Bilioni 7.4 kwa ajili ya kufanya utafiti na kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Umoja wa Ulaya umeahidi kuchangia Euro bilioni moja, Ujerumani itatoa Euro milioni 525 na Ufaransa itatenga Euro milioni 500, na Norway imekubali itachangia katika mpango huo.