UFARANSA-UHISPANIA-KOREA KUSINI-CHINA-CORONA-AFYA

Shughuli za kawaida kuanza kurejea Ufaransa na Uhispania, China na Korea Kusini matatani

Katika sekta ya uchukuzi nchini Ufaransa, uvaaji wa barakoa ni lazima, Jumatatu, Mei 11.
Katika sekta ya uchukuzi nchini Ufaransa, uvaaji wa barakoa ni lazima, Jumatatu, Mei 11. REUTERS/Benoit Tessier

Makumi ya mamilioni ya watu nchini Ufaransa na Uhispania wameanza kupata uhuru wa kutembea Jumatatu wiki hii, lakini raia wengi wana hofu ya kuzuka kwa wimbi la pili la mlipuko wa virusi hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Katika kudhibiti kabisa ugonjwa wa Covid-19, licha ya kulegeza masharti ya kutotoembea, serikali nchini Ufaransa imechukua hatua kadhaa hususan uvaaji wa barakoa ni lazima katika sekta ya uchukuzi na watu wametakia kutokaribiana kwa umbali wa mita moja.

Hatua hii ya kulegeza marufuku ya watu kutotembea inakuja baada ya majuma nane kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

Serikali ya Ufaransa inatarajia kuanza kufanya vipimo kwa wingi, huku watakaopatikana na virusi wakiwekwa karantini.

Wakati huo huo kisa cha kwanza kimethibitishwa nchini Korea Kusini na katikakati mwa China, katika mji wa Wuhan, ambako virusi hivyo vilianzia mwezi Desemba mwaka jana.

Nchi nyingi za Ulaya zimelazimika kuchukuwa hatua za kulegeza vizuizi vya kudhibiti maambukizi ya Corona kutokana na mdororo wa uchumi ambao umekuwa umeanza kuchukuwa kasi.

Wakati huo huo Shirika la Afya; WHO, lina wasiwasi ya kuzuka wimbi la pili la mlipuko wa virusi vya Corona, ambavyo vilisababisha nusu ya watu ulimwenguni kubaki nyumbani na kusababisha uchumi kudorora.

Nchini Korea Kusini, ambapo janga hili lilisababisha hasara kubwa, na serikali ya nchi hiyo kulazimika kufunga baa na kumbi za sherehe, baada ya visa vya maambukizi kuongezeka. Licha ya hatua zilizopitishwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita, visa vipya 35 vya maambukizi vimetangazwa.