SLOVENIA-CORONA-AFYA

Slovenia yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Corona

Wageni wote wanaozuru taifa la Slovenia sasa hawatahitajika kupelekwa karantini namana imekuwa ikifanyika.
Wageni wote wanaozuru taifa la Slovenia sasa hawatahitajika kupelekwa karantini namana imekuwa ikifanyika. Reuters/Srdjan Zivulovic

Serikali ya Slovenia imetangaza kukamilika kwa mlipuko wa virusi vya corona nchini humo baada ya serilai kudhibitisha chini ya visa saba kwa kipindi cha majuma mawili yaliopita,taifa la kwanza kuchukuwa hatua hiyo barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Wageni wote wanaozuru taifa hilo sasa hawatahitajika kupelekwa karantini namana imekuwa ikifanyika.

Hayo yanajiri wakati idadi ya vifo vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya Corona duniani kote imepindukia watu 300,000, ambapo vingi vya vifo hivyo vimetokea Ulaya na Marekani, tangu kuzuka kwake huko China, mwishoni mwa mwaka uliopita.

Marekani ndio yenye visa vingi kwa kuwa na vifo 85,194, ikifuatiwa na Uingereza vifo 33,614, Italia vifo 31,368, Ufaransa vifo 27,425 na Uhispania yenye vifo 27,321.

Ulaya bara ambalo limeshambuliwa vikali na virusi, ambapo mataifa kama Italia, Uhispania na Ujerumani ni miongoni mwa mengine 10 ambayo yana idadi kubwa ya maambukizi na vifo. Ujerumani inatarajiwa kuanza kuchukua hatua za kulegeza masharti ya mipakani Jumamosi, wakati mataifa mengine kadhaa ya jirani yatarajaiwa kuchukua hatua kama hizo kuanzia Juni 15.