Coronavirus: Visa vya maambukizi vyapindukia zaidi ya Milioni 8 duniani
Imechapishwa:
Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona duniani sasa imeongezeka na kufikia zaidi ya Milioni nane kote duniani wakati nchi nyingi ziliamua kulegeza masharti ya kukabiliana na janga hilo.
Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani, zinaonesha kuwa watu wengine Milioni 3 na Laki Nane wamepona huku wengine 435,662 wakipoteza maisha.
Nchi za Marekani, Brazil na Uingereza zina idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya duniani, Tedros Adhanom Ghebreysus ameonya kuwa kuna wasiwasi wa dunia kushuhudia mlipuiko mwingine wa mamabukizi haya kama ilivyoshuhudiuwa nchini China.
Mataifa kadhaa barani Ulaya yameanza kufungua mipaka yake na shyghuli za kiuchuli zimeanza kurudi taratibu.