Watu Milioni 2.16 waambukizwa Corona Marekani
Imechapishwa:
Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) nchini Marekani vimeripoti kuongezeka kwa visa 22,834 vya maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya kipindi cha saa 24 siku ya Alhamisi, na kusababisha jumla ya watu 2,155,572 ambao wameambukizwa tangu kuzuka kwa janga hilo.
Kwa upande wa vifo, virusi vya SARS-CoV-2 vimesababisha vifo vipya 754, na kufikisha jumla ya vifo 117,632.
Baadhi ya majimbo yameshuhudia kurejea upya kwa kasi ya maambukizi, wakati kiini cha mripuko huo kikiondoka kutoka jiji la New York na kuelekea Kusini na Magharibi.
Serikali imesema idadi kamili ya waliokwishaambukizwa huenda ikawa ni kubwa zaidi ya iliyochapishwa.
Wakati huo huo Ujerumani imerekodi visa vipya 504 vya maambukizi hivi leo, na kuifanya idadi ya watu waliokwishapata maradhi ya COVID-19 kufikia 188,534.