WHO-CORONA-AFYA

Shirika la Afya duniani WHO laonya kuhusu ongezeko la virusi vya Corona

Wauguzi wakiandamana wakilalamikia mazingira yao ya kazi katika kukabiliana na janga hatari la Covid-19 Afrika Kusini, Juni 19, 2020.
Wauguzi wakiandamana wakilalamikia mazingira yao ya kazi katika kukabiliana na janga hatari la Covid-19 Afrika Kusini, Juni 19, 2020. REUTERS/Mike Hutchings

Shirika la afya duniani, WHO linaonya kuendela kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona wakati huu nchi mbalimbali zinapoendelea kurejea katika hali ya kawaida.

Matangazo ya kibiashara

Ufaransa maisha yameanza kurejea kawaida na kwa mara ya kwanza kulishuhudiwa tamasha la muziki na Mamilioni ya wanafunzi wamerejea Shuleni.

Nchini Uhispania mipaka imefunguliwa na hali ya hatari kuondolewa. Hata hivyo, wakati mataifa kadhaa ya Ulaya maisha yakianza kurejea taratibu, mataifa ya Amerika Kusini yameendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi yakiongozwa na Brazil.

Kufikia sasa Brazili imerekodi visa zaidi ya milioni 1 vya maambukizi ya Corona na watu 51 407 wamefariki dunia baada ya vifo vipya 654 kuthibitishwa ndani ya muda wa saa 24 zilizopita, huku wagonjwa 579,000 wakipona ugonjwa huo hatari.