WHO-CORONA-AFYA

WHO yahitaji zaidi ya dola bilioni 30 kukabiliana na Corona

WHO inasema hatua za makusudi zinastahili kuchukuliwa kudhibiti hali hii ili kuepusha mataifa ya bara hilo kulemewa na ongezeko la virusi hivyo, wakati huu mataifa mengi yanapoanza kurejea katika hali ya kawaida.
WHO inasema hatua za makusudi zinastahili kuchukuliwa kudhibiti hali hii ili kuepusha mataifa ya bara hilo kulemewa na ongezeko la virusi hivyo, wakati huu mataifa mengi yanapoanza kurejea katika hali ya kawaida. REUTERS/Denis Balibouse/File Photo

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa dola Bilioni 31.3 (sawa na euro bilioni 27.8) zitahitajika katika miezi 12 ijayo kwa kuendesha zoezi la kufanya vipimo, matibabu na chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

WHO, ambayo ilizindua mpango wa kimataifa dhidi ya janga hili, inataka katika mfumo wa mpango huu kufanya vipimo milioni 500 na kutoa matibabu milioni 245 katika nchi zinazoendelea na zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2021, limebainisha shirika hilo katika taarifa.

Timu ya WHO pia inataka kusambaza chanjo bilioni mbili ifikapo mwisho wa mwaka wa 2021, ikiwa ni pamoja na nusu ya kiwango hicho katika nchi zenye mapato ya chini na ya kati.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani, lilisema maambukizi ya virusi vya Corona yameongezeka kwa kipindi cha wiki moja iliyopita barani Ulaya, hali ambayo inazua wasiwasi wa kuendelea kushuhudiwa kwa maambukizi mapya.

WHO inasema hatua za makusudi zinastahili kuchukuliwa kudhibiti hali hii ili kuepusha mataifa ya bara hilo kulemewa na ongezeko la virusi hivyo, wakati huu mataifa mengi yanapoanza kurejea katika hali ya kawaida.

Bara la Ulaya pekee limeripoti visa Milioni 2.6 vya maambukizi ya Corona, huku watu zaidi ya 195, 000 wakipoteza maisha.