Coronavirus: zaidi ya nusu milioni wafariki dunia
Imechapishwa:
Ulimwengu, unaokabiliwa tangu Desemba mwaka jana na janga la Covid-19, umerekodi zaidi ya vifo nusu milioni na visa milioni milioni vya maambukizi, wakati virusi hivyo vinaendelea kiathiri Marekani na China ikikabiliwa na mlipuko wa pili wa janga hilo.
Kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP kutoka vyanzo rasmi, vifo 500,390 na kesi 10,099,576 za maambukizi zimethibitishwa rasmi siku ya Jumapili.
Idadi ya vifo vilivyorekodiwa ulimwenguni kote imeongezeka maradufu katika miezi miwili tu (250,000 mnamo Mei 5) na vifo vipya 100,000 vimerekodiwa katika siku 10 zilizopita.
Ulaya ni bara lililo na vifo vingi zaidi (vifo 196,086 kwa jumla ya kesi 2,642,897 za maambukizi), ikifuatiwa na ukanda wa Marekani / Canada (vifo 134,315, kwa jumla ya visa 2,642,754 vya maambukizi), Amerika ya Kusini na Karibiani (vifo 111,640 kwa jumla ya wagonjwa 2,473, 164), Asia (vifo 33.107, kwa jumla ya wagonjwa 1.219.230), Mashariki ya Kati (vifo 15.505 kwa jumla ya 730.977), Afrika (vifo kwa jumla ya wagonjwa 9.604, 381.396) na Oceania (vifo 133 kwa jumla ya wagonjwa 9.158).
Marekani ndio nchi iliyoathiriwa zaidi, kwa idadi ya vifo (125,747) na kesi (2,539,544) za maambukizi. Ingawa idadi ya vifo vya kila siku imepungua kidogo mnamo mwezi Juni ikilinganishwa na mwezi uliopita, maambukizi yameongezeka katika majimbo 30 kati ya 50 nchini Marekani, hasa katika majimbo makubwa na yenye wakazi wengi Kusini na Magharibi mwa nchi: California, Texas na Florida.
Nchi ambayo ni ya pili kuwa na wagonjwa wengi Brazil, taifa hilo lina wagonjwa milioni 1.3 na vifo vinavyozidi 57,000.
Tangu mlipuko wa virusi hivyo nchini China mwishoni mwa mwaka jana, kumekuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 10, kulingana na Johns Hopkins.