DUNIA-CORONA-AFYA

Watu Milioni 12 waambukizwa virusi vya Corona duniani

Nchini Marekani, idadi ya watu waliombukizwa sasa imefikia zaidi ya Milioni tatu, huku watu waliopoteza maisha, idadi ikiongezeka na kufikia zaidi ya Laki Moja na Elfu Thelathini.
Nchini Marekani, idadi ya watu waliombukizwa sasa imefikia zaidi ya Milioni tatu, huku watu waliopoteza maisha, idadi ikiongezeka na kufikia zaidi ya Laki Moja na Elfu Thelathini. AFP / Nicolas Tucat

Watu zaidi ya Milioni 12 kote duniani kwa sasa wameambukizwa virusi vya Corona na wengine zaidi ya Laki Tano na Elfu 48, wamepoteza maisha kwa mujibu wa takwimu kutoka chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizi zinatolewa wakati Shirika la afya duniani WHO likionya kuwa bado kuna safari ndefu ya kulishinda janga hili ambalo limeikumba dunia.

Watu wengine Milioni 6.5 wamepona baada ya kuambukizwa huku Marekani na Brazil yakiwa mataifa mawili yenye idadi kubwa ya maambukizi na vifo duniani.

Nchini Marekani, idadi ya watu waliombukizwa sasa imefikia zaidi ya Milioni tatu, huku watu waliopoteza maisha, idadi ikiongezeka na kufikia zaidi ya Laki Moja na Elfu Thelathini.

Licha ya ongezeko hili, serikali ya rais Donald Trump inasisitiza kuwa shughuli za kawaida kama Shule kufunguliwa, zinastahili kurejelewa.

Wakati hayo yakijiri, Shirika la Kimataifa linalohusika na misaada ya Kibinadamu la Oxfam, limeonya kuwa janga la Corona litasababisha baa la njaa na kuwaathiri watu zaidi ya Milioni 120 kote duniani.