Covid-19: London yashutumu Moscow kwa kujaribu kuiba utafiti wa chanjo
Serikali ya Moscow imenakusha madai ya London kwamba maafisa wa Urusi wamejaribu kuiba utafiti ulioendeshwa na wanasayansi kutoka Marekani, Canada na Uingereza ili kupata chanjo dhidi ya virusi vya SARS-CoV-2.
Imechapishwa:
Shutma hizi mpya za London dhidi ya Moscow zinakuja kuzidisha mvutano kati ya Urusi na Uingereza na kuharibu uhusiano kati ya nchi hizi mbili.
SMarekani, Uingereza na Canada zimeituhumu Urusi katika taarifa ya pamoja ya usalama, madai ambayo Urusi imeyakanusha kupitia msemaji wa Ikulu Dmitry Peskov.
Kituo cha Kitaifa cha Usalama wa Mitandao kikasema kundi la wadukuzi kwa jina APT29 liliyalenga maabara ya Uingereza yanayofanya utafiti wa chanjo ili kuiba data muhimu za utafiti. Shirika hilo limesema lina uhakika wa zaidi ya asilimia 95 kuwa wadukuzi hao ni sehemu ya mashirika ya kijasusi ya Urusi na yanalenga kukusanya habari kuhusu utafiti wa chanjo ya Covid-19.
Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa majaribio ya chanjo inayofanyiwa utafiti na Chuo Kikuu cha Oxford yameonyesha kuwa imetengeneza kinga ya mwili dhidi ya kirusi hicho.
Kufikia sasa ugonjwa aw Covid-19 umeuwa zaidi ya watu 585,000, kuwaambukiza zaidi ya milioni 13.6 na kuuathiri uchumi wa ulimwengu tangu ulilipolipuka mwishoni mwa mwaka jana.