DUNIA-WHO-CORONA-AFYA

WHO yazitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo. REUTERS/Denis Balibouse

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeaonya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, miezi sita baada ya janga hili kuikumba dunia, wakati watu zaidi ya Milioni 18 wakiwa wameambukizwa na wengine zaidi ya 690,000 wamepoteza maisha, kote duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.

Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito kwa nchi zote kutilia mkazo hatua muhimu za kiafya ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha raia wao kuvaa barakoa, kuwataka raia wasikaribiane kwa mita kadhaa, na kuwataka kuosha mikono kila mara bila kusahau kupima virusi hivyo.

Hata hivyo WHO imeendelea kukosoa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na baadhi ya nchi duniani kwa kulegeza masharti ya kukabiliana na janga la Covid-19, ikisema kuwa Covid-19 bado ni tishio duniani.