AFRIKA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ukosefu wa vipimo katika baadhi ya nchi wapotosha idadi ya maambukizi

Afrika sasa ina kesi zaidi ya milioni moja ya virusi vya Covid-19. Lakini kulingana na wataalamu wengi katika sekta ya afya, idadi halisi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19 kwenye bara hilo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Vipimo vya Covid-19 huko Abuja, Nigeria, mnamo Aprili 2020.
Vipimo vya Covid-19 huko Abuja, Nigeria, mnamo Aprili 2020. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo tayari umegharimu maisha ya watu karibu 22,000 kwenye bara hilo, kulingana na ofisi ya kikanda ya Shirika la Afya Duniani, na idadi ya maambukizi yaliyothibitisha imezidi rasmi Milioni moja jana usiku.

Lakini kulingana na Kituo cha Umoja wa Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, zaidi ya 80% ya vipimo vya Covid vilivyofanywa kwenye bara hilo ni kutoka nchi kumi tu.

Nchi nyingi za Afrika bado hazifanyi vipimo vya kutosha, kwa sababu ya ukosefu wa uwezo au vinazuiwa na ukosefu wa usalama.

Kwa hivyo ni vigumu kugundua virusi hivyo kwa wakati muafaka. Nigeria, kwa mfano, yenye wakazi Milioni 208, nchi iliyoathiriwa zaidi ambayo ina kesi za maambukizi karibu 45,000, kufikia sasa inafanya tu vipimo 3,000 kwa siku. Kwa kulinganisha, hii ni sehemu ya kumi tu ya vipimo vya kila siku vinavyofanywa nchini Afrika Kusini.

Leo, ni nchi tano tu ndizo zinazoskusanya asilimia 75 ya kesi za maambukizi zilizothibitishwa katika bara hilo.

Afrika Kusini inaongozwa kwa visa 540,000 vya maambukizi - zaidi ya nusu ya kesi zilizoripotiwa barani Afrika - na zaidi ya vifo 9,000.

Katika orodha ya nchi zilizoathirika zaidi barani Afrika, inafuata Misri, Nigeria, Ghana na Algeria. Katika nchi hizi, idadi ya maambukizi inaanza kupungua, lakini shirika la Afya Duniani, WHO lina wasiwasi juu ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi nchini Kenya, Ethiopia na Zimbabwe. Kutokana na kutotoa majibu haraka, maambukizi ya Covid-19 kwenye bara la Afrika yanaweza kuongezeka zaidi.