URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Urusi yachukulia wasiwasi wa kimataifa juu ya chanjo ya Covid-19 kuwa 'hauna msingi'

Maafisa wa serikali ya Urusi na wafanyakazi wakivalia mavazi maalumu ya kujikinga dhidi ya Corona wakikagua abiria kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo, Moscow, Urusi, Machi 7, 2020.
Maafisa wa serikali ya Urusi na wafanyakazi wakivalia mavazi maalumu ya kujikinga dhidi ya Corona wakikagua abiria kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo, Moscow, Urusi, Machi 7, 2020. REUTERS/Stringer

Urusi imetupilia mbali kuongezeka kwa wasiwasi kutoka jamii ya kimataifa juu ya usalama wa chanjo yake ya Covid-19 iliyotengenezwa nchini humo, na kutaja kuwa wasiwasi huo "hauna msingi wowote".

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne Urusi ilisema kuwa chanjo iliyotngeza iliidhinishwa kisheria baada ya miezi isiyozidi miwili ya kufanya vipimo kwa binadamu.

Lakini wataalam wahawakuchelewa kuonyesha wasiwasi wao juu ya chanjo hiyo iliyotengenezwa haraka, na nchi zimetilia mashaka chanjo hiyo kutoka Urusi.

Wanasayansi kutoka Ujerumani, Ufaransa, Uhispania na Marekani wametoa wito wa kuwa makini kwa chanjo hiyo.

"Inaonekana kuwa wenzetu kutoka nchi za kigeni wanahisi faida maalum za ushindani wa dawa iliyotengenezwa na Urusi na wanajaribu kutoa maoni ambayo ... hayana msingi wowote," Waziri wa Afya wa Urusi Mikhail Murashko ameliambia shirika la habari la Interfax Jumatano wiki hii, huku akibaini kwamba chanjo hiyo itaanza kupatikana hivi karibuni.

"Vifurushi vya kwanza vya chanjo ... vitaanza kupatikana ndani ya wiki mbili zijazo, madaktari ndio watapewa chanjo hizo," ameongeza Bw Murashko.

Maafisa wa Urusi wametangaza kwamba wanapanga kuanza kutoa chanjo yhiyo mwezi Oktoba mwak huu.Tangazo la Jumanne lilitolewa na rais Vladimir Putin, ambaye alidai chanjo ilifanyiwa chunguzi zote zinazohitajika na kwamba binti yake tayari amepewa chanjo hiyo.

Lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema liko katika mazungumzo na viongozi wa Urusi kufanya tathmini ya chanjo hiyo, ambayo imepewa jina la Sputnik-V.