AFRIKA-ULAYA-WHO-CORONA-AFYA

Maambukizi ya virusi vya Corona yaanza kupungua Afrika

Mlipuko wa virus vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mji wa Wuhan, katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.
Mlipuko wa virus vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mji wa Wuhan, katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019. NEXU Science Communication/via REUTERS

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika imeanza kushuka kuanzia wiki iliyopita,hii ikitafsiriwa kuwa ishara nzuri ya bara hili kufanikiwa katika mapambano dhidi ya janga hili.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Dkt John Nkengasong amesema  ingawaje ugonjwa huo ulikuwa hatari ,kuna matumaini ya kuushinda.

Afrika kufikia sasa ina zaidi ya maambukizi milioni moja ,Afrika Kusini ikichangia kiasi kikubwa.

Kwa upande mwingine shirika la Afya Duniani WHO limesema bara ulaya linaweza kupambana na maambukzi mapya ya Corona pasipo kurejesha amri ya kusalia manyumbani.

Kuanzia Alhamisi, Italia, Ufaransa na Uhispania ,zimeshuhudia ongezeko la kasi ya maambukizi ya virusi hivyo.