WHO-CORONA-AFYA

Coronavirus: WHO yatarajia janga la Corona kumalizika katika kipindi cha miaka 2

Mlipuko wa virus vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulianzia katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.
Mlipuko wa virus vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulianzia katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019. INDRANIL MUKHERJEE / AFP

Shirika la Afya Duniani (WHO) linatumai kwamba janga la Corona linaweza kuwa limemalizika kabisa katika kipindi cha miaka miwili ijayo, mkurugenzi wake, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema.

Matangazo ya kibiashara

Itachukuwa miaka miwili kumalizika kabisa kwa homa ya Uhispania, ambayo ilizuka mnamo mwaka 1918, Tedros Adhanom Ghebreyesus amekumbusha.

"Hali yetu leo, kutokana na teknolojia zaidi na bila shaka mawasiliano ya hali ya juu kati ya mataifa, inaongeza uwezekano wa kuenea kwa virusi vya Corona, na kusababisha kusambaa kwa haraka," Mkurugenzi wa WHO amebaini.

"Wakati huo huo, tunayo teknolojia na maarifa ya kuizuia" , Tedros Adhanom Ghebreyesus ameongeza.

Zaidi ya watu milioni 22.8 duniani wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19 na watu 793,382 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo hatari, kulingana na takwimu za shirika la habari la Reuters.