MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus : Chanjo dhidi ya Corona kusambazwa mwishoni mwa mwezi Oktoba Marekani

Gazeti la New York Times limeripoti kwa mara ya kwanza kwamba viongozi wa CDC wamekutana na wawakilishi wa majimbo 50 na miji mikubwa mitano ili kuwapa habari juu ya ratiba hiyo.
Gazeti la New York Times limeripoti kwa mara ya kwanza kwamba viongozi wa CDC wamekutana na wawakilishi wa majimbo 50 na miji mikubwa mitano ili kuwapa habari juu ya ratiba hiyo. REUTERS

Vituo vya vya kudhibiti na kuzuia maambukizi ya magojnwa nchini Marekani (CDC) vimewataka maafisa wa afya wa majimbo yote nchini humo kuwa tayari kusambaza chanjo dhidi ya Corona kwa watu walio katika hatari kubwa mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Matangazo ya kibiashara

Suala hilo limekuwa suala la kisiasa wakati rais anayemaliza muda wake, Donald Trump, ambaye anataka kuchaguliwa tena mwezi Novemba mwaka huu, ametoa wa mabilioni ya dola kwa maabara ya dawa ili kuharakisha maendeleo ya chanjo dhidi ya COVID-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona, ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 180,000 nchini Marekani.

Gazeti la New York Times limeripoti kwa mara ya kwanza kwamba viongozi wa CDC wamekutana na wawakilishi wa majimbo 50 na miji mikubwa mitano ili kuwapa habari juu ya ratiba hiyo.

Anthony Fauci, mtaalam anayeongoza wa magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani, ameiambia televisheni ya MSNBC leo kwamba, kulingana na takwimu kutoka kwa vipimo vinavyoendelea, takwimu za kliniki za kutosha zinaweza kupatikana mwezi Novemba au Desemba ili kubaini kama moja ya chanjo iko salama na nzuri.

Kulingana na nyaraka zilizochapishwa na Gazeti la New York Times, CDC inajiandaa kuwa na chanjo moja au mbili kwa idadi ndogo mwishoni mwa mwezi Oktoba.