MAREKANI-CORONA-AFYA

Majaribio ya chanjo ya COVID-19 yasitishwa kwa muda

Maambukizi duniani kote hadi sasa  ni  zaidi ya  watu milioni 27, na zaidi  ya  watu 890,000 wamefariki kutokana  na  ugonjwa  huo.
Maambukizi duniani kote hadi sasa ni zaidi ya watu milioni 27, na zaidi ya watu 890,000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo. ANDREW CABALLERO-REYNOLDS / AFP

Majaribio ya mwisho ya chanjo ya virusi  vya Corona, yaliyokuwa yanafanywa na kampuni ya AstraZeneca na Chuo Kikuu cha Oxford yamesitishwa kwa muda baada ya mtu aliyekuwa anajaribiwa chanjo hiyo kuumwa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, AstraZeneca imetaja hatua hiyo kama ya kawaida katika mchakato wa majaribio ya chanjo, na kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuangazia tena usalama wa chanjo hiyo.

Kampuni hiyo ni miongoni mwa makumpuni tisa duniani ambayo yako mbioni kutafuta chanjo ya virusi vya Corona, kampuni hiyo ikionekana kuongoza baada ya chanjo yake kuingia katika awamu ya tatu na ya mwisho ya majaribio nchi Marekani mwishoni mwa mwezi Agosti.

Aidha, rais wa Marekani Donald Trump amesema angependa chanjo ya virusi hivyo kupatikana nchini mwake kabla ya uchaguzi wa Novemba, matamlshi yake hata hivyo yakizua wasiwasi kuwa huenda siasa zikapewa kipaumbele badala ya usalama wa upatikanaji wa chanjo hiyo.