WHO-DUNIA-AFYA

WHO yaonya kuhusu ongezeko la maambukizi ya Corona

WHO imetoa wito kwa serikali mbalimbali za dunia na viongozi wa sekta mbalimbali za kiafya kuangazia kwa umakini afya na usalama wa wahudumu wa afya na wagonjwa haswa kipindi hiki cha janga la Corona.
WHO imetoa wito kwa serikali mbalimbali za dunia na viongozi wa sekta mbalimbali za kiafya kuangazia kwa umakini afya na usalama wa wahudumu wa afya na wagonjwa haswa kipindi hiki cha janga la Corona. REUTERS/Denis Balibouse/File Photo

Shirika la afya duniani WHO linasema ongezeko la maambukizi ya Corona barani Ulaya, linatisha baada ya idadi ya watu wanaoambukizwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa mwezi Septemba.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya Hans Kluge amesema, ongezeko la maambukizi katika mataifa mbalimbali barani Ulaya, ni ishara kuwa hali inaendelea kuwa mbaya.

Kluge anataka mataifa ya Ulaya kuangalia upya hatua yao ya kulegeza zaidi masharti ya kupambana na janga hili ambalo limewaathiri watu zaidia ya Milioni Mbili na vifo zaidi ya Laki Mbili.

Wakati huo huo WHO imetoa wito kwa serikali mbalimbali za dunia na viongozi wa sekta mbalimbali za kiafya kuangazia kwa umakini afya na usalama wa wahudumu wa afya na wagonjwa haswa kipindi hiki cha janga la Corona.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, WHO limewataka wadau husika kuchukua hatua madhubuti kuwalinda wahudumu wa afya dhidi ya dhulma na maswala mengine yanayohatarisha usalama wao.