DUNIA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Zaidi ya vifo milioni vyarekodiwa ulimwenguni

Corona imeathiri mambo mengi katika nchi nyingi duniani.
Corona imeathiri mambo mengi katika nchi nyingi duniani. NEXU Science Communication/via REUTERS

Zaidi ya watu milioni wamefariki dunia ulimwenguni baada ya kuambukizwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huko Wuhan, nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, vifo 1,000,009 vimerekodiwa rasmi ulimwenguni kote, kwa visa 33,018,877 vya maambukizi. Wagonjwa 22,640,048 wamethibitishwa kupona ugonjwa huo.

Maeneo yaliyoathiriwa zaidi kwa idadi ya vifo ni Amerika Kusini na Karibiani (vifo 341,032 kwa jumla ya visa 9,190,683 vya maambukizi), Ulaya (vifo 229,945 kwa jumla ya visa 5,273,943 vya maambukizi) na Marekani na Kanada (vifo 214,031 kwa jumla ya visa 7,258. 663 vya maambukizi).

Siku ya Jumatatu India ilitangaza kuwa watu waliokwishaambukizwa virusi hivyo wamefikia milioni 6.1, ikikaribia sana kuipiku Marekani ndani ya wiki chache zijazo kwa kuwa na maambukizo mengi. Watu 100,000 wameshapoteza maisha kwa maradhi hayo ya COVID-19.

India imekuwa ikiongeza baina ya wagonjwa 80,000 hadi 90,000 kwa siku tangu ilipoanza kuripoti idadi kubwa ya maambukizo mwishoni mwa mwezi Agosti. Waziri Mkuu Narendra Modi alisema siku ya Jumapili (Septemba 27) kwamba watu wanapaswa kuendelea kuvaa barakowa wanapokuwa nje ya majumba yao.

Kirusi jamii ya SARS-CoV-2, ambacho kinahusika na maambukizo ya COVID-19, ni cha hivi karibuni kabisa miongoni mwa virusi vilivyoangamiza idadi kubwa ya watu kwenye karne ya 21.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.