WHO-CORONA-AFYA

WHO: 10% ya watu duniani wameambukizwa virusi vya Corona

Msafiri akifanyiwa vipimo vya Covid-19 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Rafik Hariri huko Beirut, Lebanon, Julai 1, 2020.
Msafiri akifanyiwa vipimo vya Covid-19 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Rafik Hariri huko Beirut, Lebanon, Julai 1, 2020. Bilal Hussein/AP Photo

Shirika la afya duniani WHO, limesema kuwa Mtu mmoja kati ya wengine 10 duniani, huenda aliaambukizwa virusi vya Corona, hali ambayo kulingana na shirika hilo bado dunia imo katika hatari ya kukumbwa na maambukizi zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa hizo, watu zaidi ya milioni 35 wamethibitishwa kuaambukizwa virusi hivyo ila linasema kuwa takwimu kamili huenda ikawa ni watu zaidi ya milioni mia nane ambao wameambukizwa.

Visa milioni 35.4 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinaripotiwa duniani kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, nchini Marekani, wakati shirika la habari la AFP linabaini kwamba watu Milioni 35.2 wameambukizwa virusi vya Corona duniani. Takwimu nyingi zinakubaliana juu ya kidadi hii kubwa. Hata hivyo, WHO imebaini kwamba watu milioni 35.1 wameambukizwa virusi vya Corona.

Kwa kile ambacho inadaiwa ni kwamba, idadi hiyo ingebidi kuzidishwa na zaidi ya 20 ili kupata wazo la kiwango cha janga hilo. Hivi ndivyo mkuu wa shughuli za dharura katika shirika al Afya Dunia, WHO, Mike Ryan anasema:

“Uchunguzi wetu wa hivi karibuni unaonyesha kuwa 10% ya idadi ya watu wanaweza kuwa wameambukizwa. Takwimu hii inatofautiana na nchi, ikiwa ni katika eneo la miji au eneo la vijijini. Lakini [ingawa mtu mmoja kati ya watu 10 ameambukizwa], maana yake ni kwamba idadi kubwa ya watu ulimwenguni bado wako hatarini. "

Hata hivyo Mike Ryan hasemi jinsi WHO imeweza kupata idadi hii.