COLOMBIA-UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kesi zaidi ya milioni moja za maambukizi zathibitishwa Colombia

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya Corona nchini Colombia imezidi milioni moja, imebaini mamlaka ya afya nchini Colombia, nchi ya nane ulimwenguni kuvuka kiwango cha juu cha watu milioni moja.

Colombia, vizuizi vimewekwa ili kuzuia janga la Corona.
Colombia, vizuizi vimewekwa ili kuzuia janga la Corona. REUTERS/Luisa Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Colombia inaendelea kukumbwa na maambukizi zaidi ya ugoinjwa hatari wa COVID-I9 katika bara la Amerika.

Hayo yanajiri wakati mlipuko mpya wa ugonjwa huo umeendelea kuyaathiri mataifa mengi katika bara la Ulaya.

Nchini Ujerumani, zaidi ya watu 10,000 wamefariki dunia nchini Ujerumani kutokana na viursi vya Corona. Wakati huo huo Kansela Merkel Merkel ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo 'kupunguza mawasiliano' ili kupunguza maambukizi zaidi.

Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI) kilirekodi watu 10,003 waliofariki dunia Jumamosi baada ya vifo zaidi 49 kuthibitishwa siku moja kabla.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.