AFYA-CORONA-MAREKANI

Financial Times-Coronavirus: Chanjo ya AstraZeneca hutoa majibu ya kinga kwa watu wazee

Ugonjwa hatari wa COVID-19 umeua watu wengi duniani.
Ugonjwa hatari wa COVID-19 umeua watu wengi duniani. REUTERS

Matokeo ya awali ya majaribio ya kliniki ya chanjo inayotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford kwa kushirikiana na kampuni ya Uingereza ya AstraZeneca dhidi ya virusi vya Corona inaonyesha kuwa hutoa majibu makubwa wa kinga kwa wazee, wale walio katika hatari ya kupata maambukizi ya COVID-19, Gazeti la Financial Times limebaini.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo yanaendana na takwimu zilizotolewa mwezi Julai ambayo yalionyesha chanjo hiyo ilitoa "majibu thabiti ya kinga" kwa wagonjwa wenye afya kati ya miaka 18 na 55, Gazeti la Financial Times limeongeza.

Gazeti la Financial Times linaonya, hata hivyo, kwamba majaribio mazuri ya kinga ya mwili hayahakikishi kuwa chanjo hiyo itakuwa salama na yenye ufanisi kwa wazee.

Maelezo ya ugunduzi huu yanatarajiwa kuchapishwa hivi karibuni katika jarida la kisayansi, Financial Times limebaini.

Siku ya Ijumaa, AstraZeneca ilitangaza kuwa imeanza tena majaribio ya kliniki yaliyofanywa nchini Marekani juu ya chanjo yake dhidi ya virusi vay Corona baada ya kupewa ruhsa na mamlaka ya afya nchini humo.