WHO-CORONA-AFYA

WHO kusaidia nchi zisizojiweza kukabiliana na kusambaa kwa COVID-19

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus kwenye makao makuu ya WHO, huko Geneva, Uswisi Julai 3, 2020.
Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus kwenye makao makuu ya WHO, huko Geneva, Uswisi Julai 3, 2020. Fabrice Coffrini/Pool via REUTERS

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni amesema zaidi ya visa laki moja vya maambukizi ya virusi vya Corona vimekuwa vikiripotiwa ulimwenguni kila siku katika wiki mbili zilizopita - haswa nchini Marekani na Asia ya Kusini - na pia kwenye nchi ambazo zimefanikiwa kusimamisha usambazaji wa Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Tedros Adhanom Ghebreyesus amebainisha kuwa WHO inafanya kila linalowezekana kufanikisha mataifa yasiyojiweza kukabiliana na kuenea kwa maambukizi mapya.

Hayo yanajiri wakati visa zaidi ya milioni 8 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa nchini India leo Alhamisi, baada ya visa vipya 49,881 kuripotiwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kulingana na takwimu ziliztolewa na Wizara ya Afya.

Wakati huo huo China imerekodi visa vipya 47 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, ikiwa ni idadi ya juu zaidi tangu miezi miwili iliyopita, Tume ya Kitaifa ya Afya imebaini leo Alhamisi katika mkutano wake wa kila siku kuhusu janga hilo.

Ongezeko la maambukizi mapya limeendelea kuripotiwa katika nchi mbalimbali za Ulaya, Amerika na Asia.