Obama akataa kuonesha picha za maiti ya Osama Bin Laden
Imechapishwa: Imehaririwa:
Rais wa Marekani Barrack Obama anasema kuwa ameamua kuwa picha za aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qeda aliyepigwa risasi na majeshi nchini Pakistani mapema juma hili hazitatolewa wazi kwa umma.
Obama ambaye leo hii anatarajiwa kuzuzru katika eneo lililoshambuiliwa la Zero square mwaka wa 2001 ametoa sababu ya kutotoa picha hizo kuwa zinaweza kuchochea machafuko na halikadhlika propaganda kutoka kwa wafuasi wa Osama swala ambalo anasema linaweza kuwa hatari kwa usalama.
Wakosoaaji wa Marekani wamekuwa wakitaka picha za Osama kutolewa wazi,ili kuthibitishwa kweli ikiwa aliyeuawa alikuwa ni Osama lakini Marekani imethibitisha kuwa ,Osama ndiye aliyeuawa na hilo limethiobitishwa na vipimo vya DNA