Pakistani-Marekani

Marekani yaahidi kuishirikisha Pakistani katika Oparesheni za kuwasaka Magaidi

REUTERS/Mian Khursheed

Pakistan na Marekani zimekubaliana kuwa zitashirikiana katika oparesheni za kuwakamata viongozi wa ugaidi duniani.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka katika wizara ya mambo ya nje ya Pakistan inaeleza kuwa makubaliano hayo yanalenga kupunguza msuguano baina ya mataifa hayo ulioibuka baada ya Oparesheni ya makomandoo wa Marelkani iliyomuua  Kiongozi wa Alqaeda Osama bin Laden.
 

Marekani imenukuliwa mara kadhaa ikisema kuwa ingawa uhusiano baina yake na Pakistan umetetereshwa ,uhusiano huo ni muhimu na wako tayari kufanya juhudi za makusudi kuunusuru.
 

Seneta mkongwe  wa Marekani John Kerry amekuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kuzuru nchini humo tangu kuuwawa kwa Bin Laden tarehe 2 Mei mwaka huu  katika eneo la Abbotabad nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo Islamabad.
 

Pakistan ilijikuta katika wakati mgumu ilipolazimika kuelezea ni kwa kwa nini vyombo vyake vya  usalama havikufahamu uwepo wa bin Laden katika ardhi ya nchi hiyo,huku Marekani nayo ikikosolewa kwa kufanya oparesheni hiyo bila ya ruhusa ya pakistan suala lililotafsiriwa kuwa ni kuingilia uhuru wa nchi nyingine.