Marekani

Idadi ya vifo vya kimbunga nchini Marekani yazidi kuongezeka

REUTERS/Mike Stone

Wakazi wa majimbo ya Marekani wameonywa kujiandaa na Kimbunga baada ya Kushuhudia jimbo la Missouri likipoteza wakazi wake mia moja kumi na sita kufuatia kimbunga kikali kurekodiwa katika kipindi cha miongo sita.

Matangazo ya kibiashara

Wataalam wa hali ya hewa wameonya kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na tukio hilo kusababisha majeruhi zaidi ya elfu moja.

Gavana wa Misouri Jay Nixon amesema vikosi vya uokoaji vinaendelea na zoezi la kuwatafuta manusura wa tukio hilo.

Hali hiyo imesababisha wasiwasi kwa wakazi wa majimbo mbalimbali nchini Marekani kufuatia kuandamwa na vimbunga vya mara kwa mara.