Marekani

Obama aahidi kulijenga upya eneo lililo athiriwa na Kimbunga

Rais Obama alipotembelea maeneo yaliothiriwa Mei 29, 2011.
Rais Obama alipotembelea maeneo yaliothiriwa Mei 29, 2011. Reuters/Jason Reed

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kimbunga ambacho kimepiga Mji wa Joplin na kuleta madhara makubwa Missouri ni janga la taifa na ameahidi serikali yake itazisaidia familia ambazo zimeathiriwa na watalijenga upya eneo hilo.Kimbunga hicho kikali kimesababisha vifo vya watu mia moja na arobaini na mbili kimerejesha kumbukumbu ya janga kama hilo ambalo lilitokea mwezi uliopita na kuacha mamia ya wananchi wakipoteza maisha. Rais Obama amesema janga hilo limekuwa baya zaidi kuikumba nchi yake katika siku za hivi karibuni na amewataka wananchi wa Joplin kufahamu kuwa dunia nzima ipo pamoja nao.