Mexico-Marekani

Kiongozi wa kundi ZETA Jesus Enrique Rejon Aguilar akamatwa nchini Mexico

Polisi nchini Mexico imefanikiwa kumkamata kiongozi wa juu wa kundi la Zeta aliyekuwa anatafutwa pia na serikali ya Marekani kwa tuhuma za mauaji ya afisa upelelezi wa nchi hiyo.

Jesus Enrique Rejon Aguilar
Jesus Enrique Rejon Aguilar AFP
Matangazo ya kibiashara

Jesus Enrique Rejon Aguilar ambaye hutambulika pia kama El Mamito alikamatwa usiku wa kuamkia jumatatu wakati akielekea kwenda kumuona mama yake katika mji wa Campeche.

Mtuhumiwa huyo ndie anatajwa kuwa muanzilishi wa kundi la Zeta ambalo limekuwa likijihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na kuendesha mapambano dhidi ya vikosi vya serikali vinavyowasaka viongozi wa makundi hayo.

Nchi ya Marekani ilitangaza kutoa dau la dola milioni moja kwa mtu ambaye atafanikisha kukamatwa kwa kiongozi huyo na kiongozi wa juu wa Zeta Heriberto Lacano.