Venezuela-cuba

Rais wa Venezuela apokelewa kwa shangwe nchini mwake baada ya kupewa matibabu nchini Cuba

Raia wa Venezuela wamemlaki kwa shwangwe Rais Hugo Chavez, aliyerejea kama shujaa kutoka Cuba alikokwenda, kufanyiwa matibabu. 

Hugo Chavez Rais wa Venezuela
Hugo Chavez Rais wa Venezuela Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa ni shangwe na vifijo, jijini Caracas hapo jana, wakati kiongozi wa taifa hilo, akiwahutubia wananchi wake, mara tu baada ya kufanyiwa upasuaji jijini Havana.
Maelfu ya raia walikusanyika ikulu, kumuona Rais Chavez, ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa takriban mwezi mmoja sasa.

Akiwa katika sare zake za jeshi, Chavez mwenye umri wa miaka 56, amewahakikishia wananchi wake kuwa atahakikisha anakabiliana na ugonjwa wa saratani, unaomsumbua.
Tarehe nane, mwezi uliopita, kiongozi huyo aliondoka nchini humo kuelekea Cuba, na siku mbili zilizofuata hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya, jambo lililozua minong'ono mingi, ikihoji uwezo wa Chavez, kuongoza taifa la Venezuela.