Iraq -Marekani

Marekani na Iraq wazungumza kuhusu uwezekano wa kuongezwa muda wa vikosi vya mrekani nchini Iraq

Reuters

Viongozi wa nchi za Iraq na Marekani wameanza mazungumzo mapya kuangalia uwezekano wa kuongezewa muda kwa vikosi vya nchi hiyo kuendelea kubakia nchini humo.  

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Marekani ilitangaza kuwa itahakikisha inaondoa asilimia kubwa ya wanajeshi wake nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.

Mazungumzo hayo yanakuja kufuatia kuzuka hofu ya uimara wa vikosi vya nchi hiyo kuweza kulinda usalama wa mali na raia pindi majeshi ya marekani yakiondoka nchini humo.

Nchi ya marekani imebakiza wanajeshi zaidi ya Elfu arobaini na sita nchini humo wanaolinda amani kwa kusaidiana na vikosi vya serikali.