Marekani

Kesi ya mkurugenzi zamani wa IMF yashinikizwa kuendelea mjini New York

Seneta wa  New York Bill Perkins, Julay 10, 2011 mjini Harlem
Seneta wa New York Bill Perkins, Julay 10, 2011 mjini Harlem AFP PHOTO/Jessica Rinaldi

Senetor wa mjini New York, makundi yanayotetea haki za wanawake na viongozi mbalimbali wa kijamii walikusanyika pamoja hapo jana kushinikiza kuendelea kwa kesi ya mkuu wa zamani wa shirika la fedha duniani, IMF, Strauss Kahn.

Matangazo ya kibiashara

Akiwa wa wawakilishi kutoka jamii ya wamarekani wenye asili ya Afrika, waislamu na jamii ya walatino mjini New York,seneta wa New York, Bill Perkins amekosoa mashtaka hayo baada ya kuwepo taarifa kuwa kesi hiyo inaweza kutupiliwa mbali kwa kuwa mwanamke aliyefungua kesi ya ubakaji dhidi ya Kahn si muaminifu katika kesi hiyo

Perkins amesema kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo kutafanya waathirika wengi kuogopa kujitokeza kwa kuhofia wenyewe kufunguliwa mashtaka,huku akitoa wito kuangalia pia kama Strauss Kahn anayoyasema yana ukweli wowote.