Syria-Marekani

Balozi wa Marekani nchini Syria aionya serikali ya Syria kufanya mabadiliko

Balozi wa Marekani nchini Syria, Robert Ford amesema ikiwa utawala wa Syria hautasikiliza matakwa ya waandamanaji juu ya kufanyika mabadiliko ya haraka wataondolewa madarakani na raia wa Syria.

courrierinternational
Matangazo ya kibiashara

Ford ametoa wito kwa Rais wa Syria Bashar Al Assad kufanya uamuzi wa kuleta mabadiliko nchini humo.

Mwanadiplomasia huyo amesema ataendelea kuzunguka nchini Syria kuonana na raia wa Syria na kudai kuwa serikali ya Syria imekuwa ikitoa ahadi zisizotekelezeka kuhusu mabadiliko ya kisiasa nchini humo na kuongeza kuwa Raia wa Syria wanahitaji mabadiliko ya kweli na si tu mazungumzo na ahadi zisizotekelezwa.

Ford ameitia udhia serikali ya Syria tangu Ijumaa iliyopita alipohudhuria maandamano makubwa mjini Hama unaodhibitiwa na upinzani wa nchi hiyo.