Marekani

Rais Obama ataka suluhu la deni la taifa lake kupatikana katika kipindi cha saa 36 zijazo

Rais wa Marekani Barrack Obama, amewaambia wabunge nchini humo kuwa anataka suluhu kuhusu deni la kitaifa linalokumba taifa hilo kwa saa 36 zijazo.

Obama akutana na wajumbe wa congress
Obama akutana na wajumbe wa congress REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Rais Obama ameyasema hayo katika mkutano wake wa tano na wabunge wa Congress, kutafuta mbinu ya kushughulikia swala hilo.

Obama anatarajiwa kuzungumzia mikutano hiyo baadaye hivi leo ,kuwaambia Wamarekani walikofikia katika mazungumzo hayo na namna ya kukabiliana na deni hilo la kitaifa.

Marekani inadaiwa na umma Dola Bilioni 14 nukta tatu deni ambalo linastahili kulipwa kufikia Agosti tarehe mbili,na ikiwa hilo halitafikiwa uchumi wa Marekani huenda ukaporomoka na hivyo kulazimu Mareakni kubana matumizi ya fedha na hata kusabisha baadhi ya watu kupoteza kazi.,