Iran-Marekani

Raia 2 wa Marekani waachiwa huru kutoka Iran

Shane Bauer (G) et Josh Fattal
Shane Bauer (G) et Josh Fattal Reuters/Press TV/Files

Wanaume wawili raia wa Marekani,waliokuwa wamepewa kifungo cha miaka minane jela,mwezi huu kwa makosa ya kuifanyia Marekani Ujajususi nchini Iran wameaachiliwa huru.

Matangazo ya kibiashara

Shane Bauer na Josh Fattal wamekuwa wakizuiliwa tangu mwaka wa 2009 baada ya kuvuka mpaka kutoka Iraq ,baada ya kutuhimiwa kuwa wajasusi wa Mareakani, tuhuma ambazo wamekuwa wakizipinga kwa kusema kuwa walifika Iran kwa matembezi tu.

Wawili hao ,wamewasilishwa katika ubalozi wa Sweden, inayowakilisha serikali ya Marekani mjini Tehran.

Wakili wao Masoud Shafii anasema kuwa ,raia hao wameachiliwa kwa faini ya Dola Laki Nne .