Bolivia

Rais wa Bolivia aahirisha mpango wake wa ujenzi wa barabara katika misitu ya Amazon

Rais wa Bolivia, Evo Morales.
Rais wa Bolivia, Evo Morales. © Reuters

Rais wa Bolivia Evo Morales ametangaza serikali yake kuahirisha mpango wa ujenzi wa barabara katika misitu ya Amazon muda mchache baada ya kushuhudia polisi wakipambana na waandamanaji wanaoipinga mpango huo.

Matangazo ya kibiashara

Akitangaza uamuzi huo rais Morales amesema kuwa baada ya kuwepo kwa mvutano kuhusu ujenzi wa barabara hiyo inayopita katika hifadhi ya taifa ya isiboro ameamua kuahirisha mkakati huo wa serikali kwa lengo la kupitiwa upya.

Juma hili maelfu ya wananchi pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo waliandamana kushinikiza serikali kusitisha mpango huo hatua iliyoshuhudia waziri wa ulinzi Cecilia Chacon akijiuzulu kutokana na maandamano hayo.