Pakistani-Marekani

Marekani yaitaka Pakistani kuchukua hatuwa za haraka za kuangamiza mtandao wa Haqqani

Reuters/Naseer Ahmed

Serikali ya Marekani imezidisha shinikizo kwa Pakistani ikiitaka nchi hiyo kuchukua hatua za haraka kuuangamiza Mtandao wa Haqqani ambao unatuhumiwa kutekeleza shambulizi kwenye Ubalozi wa nchi hiyo huko Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Serikali Jay Carney amesema serikali ya Pakistan inatakiwa kushughulikia wale wote ambao wanauhusiano na Haqqani waliopo katika nchi yao ili kuzuia mashambulizi zaidi yanayoweza kutokea.

Serikali ya Marekani imekuwa ikitoa tuhuma nzito dhidi ya Mtadao wa Haqqani ya kwamba ndiyo uliofanya mashambulizi katika Ubalozi wake huko Kabul tarehe kumi na tatu ya mwezi huu pamoja na kushambulia Kituo cha Kijeshi cha NATO kilichopo Afghanistan.