Syria-Marekani

Syria yaituhumu Marekani kuchochea ghasia nchini humo

Maandamano katika jiji la  Homs September 27, 2011.
Maandamano katika jiji la Homs September 27, 2011. REUTERS/Handout

Wizara ya nchi za kigeni ya Syria, inatuhumu Marekani kwa kuchochea machafuko nchini humo kwa kutumia makundi ya wapiganaji.

Matangazo ya kibiashara

Wakati tuhma huizo zikitolewa, wafausi wa rais Bashar Al-Asaad wamemzuia Balozi wa Marekani nchini humo Robert Ford, na kumvamia kwa kumrusia nyanya wakati alipouwa ankutana na viongozi wa vyama vya upinzani nchini humo mjini Damascus.

Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanahisi kuwa, hatua hiyo inaashiria wazi kupagaranyika kwa maswla ya kidiplomasia kati ya Marekani na Syria, hali inayoelezwa kuwa dalili ya hali ngumu ya ushirikaino kati ya mataifa haya mawili katika siku zijazo.