Marekani

Watu 12 wauawa nchini Marekani kutokana na theluji

Hali inayoendelea nchini Marekani
Hali inayoendelea nchini Marekani lefigaro

Idadi ya watu ambao wamepoteza maisha Kaskazini Mashariki mwa Nchi ya Marekani kutokana na eneo hilo kukumbwa na dhahma la kuanguka kwa theluji imefikiwa watu kumi na wawili wakati huu hali ikiendelea kuwa mbaya.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka katika maeneo ya Massachusetts na New Jersey wameendelea kutoa onyo kwa wananchi kuwa makini kwani msimu wa theluji bado utaendelea na hata muda mwingine huduma kama za umeme huenda zikakosekena.

Watumiaji wa barabara na hata usafiri wa garimoshi za umeme wametakiwa kuwa makini kwani ni wazi huenda wakaendelea kukabiliwa na wakati mgumu zaidi kwani kiwango cha kuangukwa kwa theluji kimezidi mwaka huu.