Colombia

Kiongozi wa kundi la FARC nchini Colombia auawa

Kiongozi wa FARC akizumgumza na waandishi habari wakati wa uhai wake mwaka 2001
Kiongozi wa FARC akizumgumza na waandishi habari wakati wa uhai wake mwaka 2001

Viongozi nchini Colombia wamethitisha kufaanikiwa kumuuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji la FARC Alfonso Cano. Kulingana na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Alfonso Cano aliauwa katika mashambulizi ya jeshi la Kolombia. Hili ni pigo kubwa kwa kundi hili la FARC ambalo tangu mwaka 2008 lilikuwa halijapata pigo kama hili.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo anaejulikana kwa jina halisi kama Guillaume Leon Saenz alikuwa akisakwa tangu miezi kadhaa katika maeneo ya milima ya jimbo la Cauca ambako alijificha na kujikuta katika matatizo ya kushindwa kuondoka.

Kifo cha kiongozi wa kundi hilo ni ushindi mkubwa kwa jeshi la Colombia. Alfonso Cano alianzisha tena harakati za kundi hilo baada ya kudhoofika wakati wa ukombozi wa Ingrid Betancourt mwanamama raia wa Colombia mwenye asili ya Ufaransa mwaka 2008. Matukio kadhaa ya kundi hilo yaliripotiwa hapa na pale nchini humo.

Bila shaka kifo chake kinadhohofisha kabisaa kundi ambalo lilikuwa katika hali ngumu, kwani idadi ya wapiganaji wakundi ilitoka kwenye elfu kumi na saba hadi elfu nane na mia tano ambao sasa wamempoteza kiongozi wao