MAREKANI

Obama awa mbogo kwa wanasiasa kushindwa kufikia muafaka kuhusu ulipaji wa deni la taifa

Rais wa Marekani Barrack Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama Reuters

Marekani imeendelea kujikuta kwenye wakati mgumu baada ya Kamati Maalum ya Wanasiasa wa taifa hilo kushindwa kuafikiana juu ya mpango wa kuondoa hasara ya dola trilioni moja nukta mbili inayoikabilia nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mjadala ulikuwa mkubwa kwenye Kamati hiyo huku ubishani ukijitokeza pale ambapo wengi wametakwa matumizi yapunguzwe kwenye pande zote yaani sekta ya ulinzi na hata zile sekta zisizo za ulinzi.

Rais wa Marekani Barack Obama amekuwa mbogo na kuwashushia lawama wazi wazi wajumbea kutoka Chama Cha Republican ambao wapo kwenye Kamati hiyo kwa kuchangia kushindwa kufikiwa muafaka.

Nchi hiyo imeendelea kuwa katika siasa za nvutano hasa baada ya wanasiasa wa vyama vya Republican na Democrats kuendelea kushindwa kuafikiana kuhusu mpango wa kukabilina na deni la taifa la nchi hiyo.

Itakumbukwa vyema kati kati ya mwaka huu rais Barack Obama alijikuta katika wakati mgumu pale mapendekezo yake ya kubana matumizi na kupunguza deni la taifa yalipokataliwa mara kadhaa na bunge la Seneti.