Mexico

Serikali ya Mexico na makabiliano na wauzaji wa dawa za kulevya

Jeshi la Mexico limegundua mbinu za wauza mihadharati wanaotumia samaki wakubwa kuficha bidhaa hiyo
Jeshi la Mexico limegundua mbinu za wauza mihadharati wanaotumia samaki wakubwa kuficha bidhaa hiyo RFI

Serikali nchini Mexico imelazimika kutuma wanajeshi wake elfu nane katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo kudhibiti machafuko yanayofanywa na makundi ya wauzaji wa dawa za kulevya.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Mexico imelazimika kuchukua hatua hii ili kuweza kudhibiti matendo maovu ambayo yamepangwa kufanye na wuzaji hao wa dawa za kulevya kipindi hiki cha kuelekea sherehe za mwaka mpya.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Jose Juarez amesema wamelazimika kuongeza idadi ya vikosi vyao kutokana na kutokea kwa mauaji ya watu kumi na mmoja yaliyotokea mwishoni mwa juma lililopita.