Marekani

Mitt Romney ajigamba kumuangusha Obama katika uchaguzi mkuu wa urais

Mgombea wa chama cha republican  Mitt Romney
Mgombea wa chama cha republican Mitt Romney

Licha ya kushinda majimbo matano ya uchaguzi kuelekea kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa na chama chake cha republican kama mgombea wa urais kwenye uchaguzi ujao, mgombe Mitt Romney ameendelea kusisitiza kumuangusha rais Obama kwenye uchaguzi mkuu wa Urais.

Matangazo ya kibiashara

Mgombea huyo amefanikiwa kushinda tena kwenye miji ya cennecticut, delaware, New York, Pennsylvania na visiwa vya Rhodes ilitosha kumpa ushindi aliokuwa anautarajia ili kuweza kuteuliwa na hama chake kuwania urais.

Mitt amesema kuwa walichokifanya wananchi wa majimbo hayo ni ishara osha kuwa wanaona anafaa kupambana na rais Obama na kuahidi hata kabla hajachaguliwa kuwania kiti hicho kuwa atafanyia makbwa nchi yake.

Wagombea wengine waili waliobaki kwenye kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Newt Gingrich na Ron Paul ambao licha ya kuonekana kushindwa kwenye kinyang'anyiro hicho wachambuzi wa mambo wanasema kuwa watamuunga mkono Mitt Romney.