Pakistani-Marekani

Mazungumzo ya Pakistani na Marekani ya kwama

Eneo la Karachi, lori zinazo safirisha mafuta ya vikosi vya NATO.
Eneo la Karachi, lori zinazo safirisha mafuta ya vikosi vya NATO. REUTERS/Athar Hussain/Files

Maaafisa wa serikali wa Marekani wanarudi nyumbani baada ya mkutano wao na wawakilishi wa serikali ya Pakistan wa kuitaka Pakistan kufungua tena mpaka wake na Afganistan ili kuruhusu majeshi ya NATO na vifaa vyao majeshi hayo kupitia katika mpaka wao kwenda Afgansitan kutozaa matunda.

Matangazo ya kibiashara

Kukwama kwa mazungunzo hayo yanahatarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia kati ya Washington DC na Islamabad, baada ya mazungumzo hayo kuvunjika katika kipindi cha  wiki sita za mashauriano.

Pakistan ilifunga mpaka wake mwezi Novemba mwaka uliopita ili kuzuia majeshi ya NATO kuendelea kutumia mpaka huo kusafirisha vifaa vyao hadi nchini Afghnaistan wanakolinda usalama na kupambana na kundi la kigadii la Taliban.

Pakistani ilichukuwa hatuwa hii baada, baada ya majeshi ya NATO kutekeleza shambulizi la anga katika mpaka huo na kusabibisha mauaji ya wanajeshi 24 wa Pakistan, tukio ambalo NATO ilisema lilitekelezwa kwa makosa.

Uhusiano wa nchi hizi mbili uliendelea kudhoofika zaidi wiki iliopita pale kamanda wa majeshi ya Pakistani alikataa kumpokea kwa mazungumzo kiongozi nambari mbili wa majeshi ya Marekani, ambae alisafiri kutoka Marekani kwa ajili ya kujadili na viongozi wa pakistani kuhusu mzozo huo.

Serikali ya Islamabad imeweka ngumu zaidi katika kupandisha maradufu kiwango kilichokuwa kikitozwa kwa kila lori inayoingia kupitia njia hiyo, jambo ambalo linapelekea NATO kuendelea kutumia ndege zake katika kusafirisha vifaa vyake, na njia hi yaonekana kuwa ghali zaidi.

Washington imeondowa wajumbe wake kwenye mazungumzo na pakistani, lakini imesema  wanachukuwa mapunziko kidogo, mazungumzo yataendelea.