Marekani-Uchaguzi

Obama ajiweka sawa katika mdahalo wa pili na mgombea mwenza Mitt Romney

Barack Obama na  Mitt Romney, wakati wa mdahalo wa pili uliofanyika Hempstead, octoba 16, 2012.
Barack Obama na Mitt Romney, wakati wa mdahalo wa pili uliofanyika Hempstead, octoba 16, 2012.

Zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya kuitishwa uchaguzi mkuu nchini Marekani, wagombea Barack Obama na Mitt Romney wamechuana jana katika mjadala ulioonyeshwa moja kwa moja kwenye luninga. Mdahalo huo umeshuhudiwa na wapiga kura wengi wa Marekani siku kumi na tano baada ya wagombea hao kukutana tena ana kwa ana katika mjadala kama huo.

Matangazo ya kibiashara

Barack Obama alionekana mwenye wasiwasi kidogo, wakati mgombea wa Republican akionekana katika hali yake nzuri, ambayo imemwezesha kupanda katika kura ya maoni huo. Lakini hata hivyo mjadala huu mpya huwezi kuulinganisha na uliopita.

Hakika mjadala wa jana ulikuwa ni tofauti kabisa na uliofanyika Denver, siku kumi na tano zilizopita, muundo wake na uendeshwaji wake ambapo wapigakura ndio waliouliza maswali baada ya kuchaguliwa na waandishi wa habari waliosimamia na kuendesha mjadala. Wagombea hao wawili wali walitowa majibu moja kwa moja kwa jopo la wapiga kura na kuonekana wenye kazi kubwa

Barack Obama ilionekana mwenye kushambulia zaidi kuliko mjadala wa kwanza, na kusimama katika kiti chake kumsogelea karibu mgombea mwenza Mitt Romney ambaye alikuwa na neno, na kumkata kuzungumzia kinyume na alivyokuwa akizungumzia. Wagombea hao wawili wamepambana vikali na kugusia maswala mbalimbali yakiwemo sekta ya mafuta, mikakati ya kodi na shambulio katika ubalozi wa Marekani jijini Benghazi, nchini Libya, ambapo Wamarekani wanne waliuawa, akiwemo Balozi Chris Stevens.

Bila kumshambulia mwenzie, Barack Obama ameonekana kuwa mpambanaji zaidi kuliko alivyokuwa katika mjadala wa Denver mwanzoni mwa mwezi huu.

Wagombea hao wawili kila mmoja ameonyesha mtazamo wake kuhusu hatma ya taifa la Marekani katika miaka ijayo huku wakigusia maswala kadhaa ya kimataifa.

Barack Obama alikuwa anasubiriwa na wengi. Alitakiwa kuonyesha mapambano, jambo ambalo alifaulu kilionyesha bila hata hivyo kuleta madhara ya uchochezi dhidi ya mgombea mwenza. Mbele ya Obama Mitt Romney hakuonekana mwenye kushindwa ingawaje hakuwa juu kama ilivyokuwa katika mdahalo uliotangulia

Omaba alionekana mwenye furaha zaidi kuliko Mitt Romney.
Mjadala mwingine kama huo utafanyika siku ya jumatatu ijayo jijini Floride. Wagombea hao wawili wanaendeleza kampeni zao za uchaguzi. Obama anaelekea Iowa na Ohio, wakati Mitt Romney akielekea Virginia