MAREKANI

Kiongozi wa kijeshi wa Marekani ataka wanajeshi zaidi ya elfu 13 kubaki nchini Afghanistan.

Kiongozi wa juu wa kijeshi nchini Marekani, Jenerali James Mattis ameshauri kubaki vuya wanajeshi 13, 600 wa Marekani nchini Afghanistan baada ya kuondoka kwa vikosi vya NATO mwaka 2014.

Jenerali James Mattis
Jenerali James Mattis commons.wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza Kiongozi wa Kijeshi anashauri juu ya Idadi ya wanajaeshi watakaobaki nchini Afghanistan wakati huu ambapo Uongozi wa juu nchini Marekani uanajadiliana juu ya idadi ya wanajeshi wanaotakiwa kubaki ifikapo mwaka 2014.

Mattis amesema kuwa Vikosi hivyo vya marekani vitaungana na Wanajeshi kadhaa ambao si wa NATO ambao ni takriban asilimia 50 ya watokao Marekani.

Mapendekezo ya Mattis yanaonesha kuwa Jeshi linataka sehemu kubwa ya Jeshi la Marekani kuendelea kubaki nchini Afghanistan baada ya mwaka 2014 kuliko ambavyo imekuwa ikipendekezwa na Maafisa wa Ikulu kwa kutaka sehemu ndogo tu ya jeshi.