VENEZUELA

Rais wa Venezuela afariki dunia

Rais wa Venezuela, Hugo Chavez amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Saratani kwa muda mrefu. 

Rais wa Venezuela Hugo Chavez enzi za uhai wake
Rais wa Venezuela Hugo Chavez enzi za uhai wake worldnews.nbcnews.com
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa Rais Nicolas Maduro ametoa taarifa za kifo cha Kiongozi huyo, na kusema kuwa askari wa Usalama wamesambazwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha usalama unaimarika.

Maduro ametangaza juma moja kuwa la maombolezo huku kukitangazwa kuitishwa kwa uchaguzi ndani ya siku 30

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Balozi wa Urusi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin wameeleza masikitiko yao kuhusu kifo hicho huku Churkin akimtaja Chavez kuwa kiungo muhimu cha mahusiano kati ya Urusi na Venezuela.

Chavez alikuwa akipata matibabu ya Saratani baada ya kuwa nchini Cuba kwa kipindi cha miezi miwili, ambapo mwezi Desemba alifanyiwa upasuaji wa mara ya nne.