MAREKANI

Marekani yatoa onyo jipya kwa Syria kuhusu matumizi ya silaha za kemikali

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama REUTERS/Larry Downing

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa onyo jipya kwa serikali ya Syria na kusema kuwa matumizi ya silaha za kemikali ni sawa na kubadilisha mchezo wakati huu ambapo Marekani inakabiliwa na shinikizo kubwa katika ardhi yake na mataifa ya nje kuhusu kuingilia kati mzozo huo wa Syria. 

Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya maafisa wa Marekani kusema kuwa wanahisi kuwa silaha hizo za kemikali tayari zimekwisha kutumika katika mashambulizi madogo madogo, rais Obama ameonya kuwa Washington lazima ichukue hatua za busara, nakubainisha ukweli wa namna gani na kwa wakati gani silaha hizo zilitumika.

Obama, ambaye awali alimwambia rais wa Syria Bashar al Assad kuwa matumizi ya silaha za kemikali yatachora mstari wa hatari na kuahidi Marekani na jumuiya ya kimataifa kufanya uchunguzi wa kisayansi katika ripoti hii ya hivi karibuni.